Standard Digital News - Radio Maisha | MISHAHARA: KNUT Yaonya Dhidi Ya Walimu Kunyimwa Mishahara
Kipindi cha sasa Maisha Jioni

MISHAHARA: KNUT Yaonya Dhidi Ya Walimu Kunyimwa Mishahara

Posted on 9:30am, Monday 29th July 2013

Related News

Na Mate Tongola

Chama cha walimu nchini KNUT kimeionya serikali dhidi ya kutowalipa walimu mishahara yao ya mwezi Julai pamoja na marupurupu yao ya usafiri kuambatana na makubaliano na serikali kabla ya kusitisha mgomo wa walimu.

Mwenyekiti wa KNUT Wilson Sossion ameitahadharisha serikali dhidi ya kuwanyanyasa walimu walioshiriki mgomo huo uliosambaratisha shughuli za masomo katika shule za umma nchini kwa takriban majumaa matatu.

Chama hicho kimesema hayo wakati waziri wa elimu Jacob Kaimenyi akisisitiza kwamba serikali haitowalipa walimu walioshiriki mgomo. Aidha tume ya mishahara ya watumishi wa umma SRC imeiandikia barua tume ya huduma za Walimu TSC ikiitaka kutowalipa walimu hao mishahara ya mwezi Julai.

Comment Policy
comments powered by Disqus