Standard Digital News - Radio Maisha | WALIMU: SRC Yaitaka TSC Kutowalipa Walimu Waliogoma
Kipindi cha sasa Staarabika

WALIMU: SRC Yaitaka TSC Kutowalipa Walimu Waliogoma

Posted on 7:40am, Wednesday 24th July 2013

Related News

Na Mate Tongola

Mzozo umeibuka kati ya Tume ya Huduma za Walimu TSC na Tume ya Mishahara, SRC. Hii ni baada ya SRC kuionya TSC dhidi ya kuwalipa walimu mishahara ya mwezi Julai, walimu walioshiriki mgomo.

Inaarifiwa kwamba mwenyekiti wa SRC Sarah Serem ameiandikia barua TSC akitoa agizo hilo, siku moja tu baada ya Chama cha Walimu Nchini KNUT kutia saini mkataba kati yake na serikali.

Hatua hii huenda ikatatiza pakubwa uhusiano kati ya serikali na viongozi wa KNUT ambao mapema wiki hii wametozwa faini ya shilingi milioni moja kwa kupuuza agizo la mahakama la kuwataka kusitisha mgomo wa walimu.

Haya yanajiri  wakati Waziri wa Elimu Prof. Jacob Kaimenyi ametangaza kwamba shule zote za msingi na za upili, zitafungwa juma moja zaidi ya muda wa kawaida ili kufidia vipindi vya masomo vilivyopotezwa kutokana na mgomo huo. Shule hizo sasa zitafungwa tarehe 16 Agosti badala ya tarehe 9.

Comment Policy
comments powered by Disqus