PODCASTS

Habari

  • Uchujaji

    Rawal na Koome wakwepa shoka la uchujaji

    Majaji Mohamed Ibrahim wa Mahakama ya Juu na Roselyn Nambuye wa Mahakama ya Rufaa watajujwa upya. Uamuzi huo umetolewa na bodi ya uchujaji wa majaji baada ya rufaa zao kwa bodi hiyo kukubaliwa. Majaji hao wawili walikuwa miongoni mwa Majaji waliotajwa kutofaa kuhudumu katika idara mpya ya Mahakama kwenye ripoti ya bodi ya uchujaji majaji iliyotolewa mwezi Agosti Mwaka huu. Bodi hiyo inayoongozwa na mjuzi wa sheria Sharad Rao aidha imetupilia mbali rufaa ya jaji Jean Gacheche. Jaji Jeanne Gacheche alitimuliwa kwa kudaiwa kuonyesha mapendeleo kwenye kesi za masuala ya bima. Aidha bodi hiyo imewataja majaji wa Mahakama ya Rufaa Kalpana Rawal na Martha Koome kufaa kuhudumu kwenye Mahakama ya rufaa. Uamuzi kuwahusu majaji hao ulifaa kutolewa mwezi Agosti lakini ukacheleweshwa kwa kuwa majaji hao walikuwa wakisikiza rufaa kuhusu tarehe ya uchaguzi.

    0 Responses

    Posted on September 21, 2012 na Tabitha Rotich

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining