Utawala
Ole Metito, Ababu, Mbadi wateuliwa mawaziri
Rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga wametangaza Mabadiliko katika baraza la mawaziri. Katoo Ole Matito sasa ndiye waziri wa usalama wa taifa wadhfa uliokuwa ikishikiliwa na marehemu Pro. George Saitoti. Ole Metito alikuwa akishikilia wadhifa wa waziri msaidizi wa ustawi wa maeneo.
Mbunge wa Budalang’i Ababu Namwamba ameteuliwa kuwa waziri wa michezo. Aliyekuwa waziri wa michezo Paul Otuoma amehamishwa hadi wizara ya serikali za wilaya wadhifa uliocha baada ya Musalia Mudavadi kujiuzulu alipokihama chama cha ODM. Alfred Khangati ambaye alikuwa waziri msaidizi katika ofisi ya waziri mkuu, sasa atashikilia wadhfa wa naibu waziri wa usalama wa taifa ambao ulikuwa ukishikiliwa na marehemu Orwa Ojode.
Mbunge wa Gwasi John Mbadi sasa ni naibu waziri katika ofisi ya wazri mkuu.
Naye James Gesami amerejeshwa katika wadhifa wake wa awali wa waziri msaidizi wa afya ya umma na matibabu baada ya mahakama kumwondolea tuhuma za ufisadi.
Posted on September 20, 2012 na Carren Omae
