NHIF
Wakenya kutozwa zaidi kwa NHIF
Wakenya watagharamika zaidi kulipa hazina ya matibabu NHIF. Akitoa tangazo hilo afisini mwake, Waziri wa huduma za matibabu Profesa Anyang' Nyong'o amesema kuwa ada ya matozo ya NHIF itaongezeka rasmi kuanzia tarehe mosi mwezi ujao kama ilivyoratibiwa kwenye gazeti rasmi la serikali. Aidha, Nyong'o amesema kuwa hatua hiyo imeafikiwa kama njia mojawapo ya kuboresha huduma za matibabu nchini. Hata hivyo, Waziri huyo amewahakikishia wananchi kuwa hakutakuwa na pingamizi kama ilivyoshuhudiwa mwaka jana ambapo mpango huo ulipingwa vikali na muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini COTU na FKE. Kuhusu suala la mgomo wa madaktari, Nyongo'o amewahimiza madaktari wanaogoma kutii uamuzi wa mahakama.
Posted on September 14, 2012 na Ali Haji Kipapuro
