PODCASTS

Habari

  • Siasa

    Uhuru aendeleza mashauri

    Siku moja tu baada ya kupata uungwaji mkono wa vyama vyenye mizizi mkoani Kati na eneo la Mlima Kenya, Naibu Waziri mkuu Uhuru Kenyatta amefanya mkutano na vyama vya Party Of Action( POA) cha Raphael Tuju, New Ford Kenya chake Eugene wamalwa, na Wiper Democratic Movement (WMD) kuanza mchakato wa kubuni muungano wa kabla ya uchaguzi mkuu. Akizungumza kwa niaba ya waliohudhuria mkutano huo kiongozi wa POA Raphael Tuju amesema wamekubaliana kubuni jopo litakalofanya mazungumzo na wawaniaji wengine walio na maono sawa ili kupata muungano wa kabla ya uchaguzi mkuu. Tuju amesema maafikiano ya vyama hivyo yatatolewa kabla ya kumalizika makataa ya Sheria ya uchaguzi kuhusu mikataba ya makubaliano. Waliohudhuria mkutano huo ni mwakilishi wa New Ford Kenya Eugene Wamalwa, kiongozi wa Alliance Party Kiraitu Murungi , mwakilishi wa WIPER Mohamed Afey, kiongozi wa POA Raphael Tuju na kiongozi wa TNA Uhuru Kenyatta.

    0 Responses

    Posted on August 9, 2012 na Bernard Oginga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining