Mzozo
Mafuta; Kenya yajiondoa kwenye mkataba na Iran
Saa chache baada ya balozi wa Marekani nchini Kenya kusema kwamba Marekani huenda ikaiwekea Kenya vikwazo baada ya kusaini mkataba wa kununua mafuta kutoka Iran, Serikali ya Kenya imetangaza kufutilia mbali mkataba huo na Iran. Katibu katika Wizara ya Kawi Partick Nyoike amesema iwapo serikali itaendelea na mkataba huo huenda ikaibua masuala baina yake na mataifa mengine. Kenya ilikuwa imetia sahihi mkataba kununua tani milioni 4 za mafuta ghafi kila mwaka kutoka Iran. Awali akijibu maswali ya wanahabari kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 236 ya uhuru wa Marekani, balozi wa Marekani nchini Kenya anayeondoka Scot Gration amesema kuwa Serikali ya Marekani inatathmini kwa kina uhusiano kati yake na Kenya kutokana na hatua ya Kenya
Posted on July 4, 2012 na Geofrey Mung'ou
