Darubini 1.
Jirongo na Ikulu
Mbunge wa Lugari ambaye pia ni mgombea urais Cyrus Jirongo amechochea ndimi za moto. Hii ni kutokana na madai yake kuwa vipo vyama kadhaa vya siasa vinavyofadhiliwa na serikali. Kauli hii imeifanya Ikulu ambayo aghalabu huhusishwa na ukimya, kutuma taarifa kwa vyombo vya habari kupinga madai hayo, na kumtaka Jirongo afyate ulimi wake. Je, madai ya Jirongo yana uzito unaoweza kuaminiwa? Ni kwa nini ameyatoa madai haya. Ndilo suala tunalolipa mwanga kwenye darubini yetu jioni ya leo. Geoffrey Mung'ou anafungua darubini hiyo.
Posted on June 27, 2012 na Geoffrey Mung'ou
