Siasa
Ikulu yamkosoa Jirongo
Katika hatua isiyo ya kawaida Ikulu ya rais nchini Kenya imemkosoa vikali mmoja wa wanasiasa waliotangaza azma ya kugombea urais. Kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari ambayo imesainiwa kwa herufi PPS Ikulu inamtaka mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo kukoma kuihusisha kwenye njama za siasa nchini. Ikulu imesema haihusiki katika ufadhili wa wanasiasa waliotangaza nia ya kugombea urais nchini. Imesema haitayachukulia matamshi ya Jirongo kwa uzito kwa kuwa historia yake siasani inajulikana kote nchini. Katika siku za hivi karibuni mbunge huyo wa Lugari ameibuka na madai kwamba baadhi ya wanasiasa waliotangaza nia ya kugombea kiti cha urais wanafadhiliwa na wenye nguvu serikalini ikiwa ni njia moja ya kuwazuia wenzao kupata kiti cha urais
Posted on June 26, 2012 na Wellingtone Nyongesa
