Ajali
Karatina;Helikopta yashindwa kupaa
Wasiwasi umekumba eneo moja la mji wa Karatina baada ya ndege ya HELIKOPTA kutua kwa ghafla kufuatia hali mbaya ya anga katika eneo hilo. Wanahabari wetu wa eneo la mlima Kenya wamesema kwamba ndege hiyo ni ya mlowezi kwa jina Allan Root ambaye alikuwa akipaa kuwaleta wanawe hapa Nairobi katika shule ya BANDA. Mtu huyo anaishi eneo la Mbuga ya LEWA na alipofika eneo la Karatina amelazimika kutua kwa ghafla katika shamba moja eneo la Mathaithi karibu na Karatina kufuatia hali mbaya ya anga. Kisa hicho kimeibua wasiwasi hasa baada ya mawaziri wawili na polisi wanne kuangamia kwenye ajali ya Helikopta wiki moja iliyopita
Posted on June 19, 2012 na Sofia Chinyezi
