Ukeketaji
Kero la Ukeketaji Narok
Visa 40 vya ukeketaji viliripotiwa mwaka jana katika eneo la Nairegia Enkare Wilayani Narok Kaskazini. Wengi wa wasichana hata hivyo waliokolewa na kupelekwa katika vituo mbalimbali katika eneo hilo, ili kupewa hifadhi. Afisa mkuu wa elimu katika eneo hilo Eunice Njuguna amesema wasichana hao walipaswa kuozwa baada ya kupashwa tohara hali inayosababisha ongezeko la idadi ya wasichana wanaoacha masomo wakiwa na umri mdogo. Njuguna amekashifu utamaduni huo akisema umepitwa na wakati, mbali na kuwa hatari kwa afya za mtoto wa kike.
Posted on June 17, 2012 na Velmah Mrenje
