PODCASTS

Habari

  • Mahakamani

    COFEK yawasilisha kesi kupinga uchujaji wa makatibu wa wizara

    Shirika la Kutetea Maslahi ya Watumizi Bidhaa - COFEK limewasilisha kesi mahakamani kupinga jinsi shughuli ya kuwachuja makatibu wa wizara ilivyoendeshwa. Kupitia wakili wake Henry Kurauka, Shirika hilo limeambia mahakama kuwa tume ya huduma za umma PSC ilikiuka sheria katika uendeshaji wa shughuli hiyo. Katibu wa COFEK Stephene Mutoro ameiambia Radio Maisha kwamba PSC ilidinda kujibu barua ya COFEK kutaka PSC kujumuisha umma katika shughuli hiyo. Aidha COFEK imeiambia mahakama kuwa PSC haikuchapisha majina ya waliowasilisha maombi ya nyadhifa hizo. Kadhalika COFEK imedai kuwa PSC imewasilisha majina 66 ya waliopendekezwa kwa Rais. Jaji Isaack Lenaola ameagiza kusikizwa Jumatano tarehe 22 mwezi huu wa Mei.

    0 Responses

    Posted on May 21, 2013 na Carren Omae

  • Mahakamani

    Mashahidi dhidi ya Wetangula Watishiwa

    Mashahidi katika kesi iliyowasilishwa mahakamani na aliyekuwa waziri wa serikali za wilaya Musikari Kombo kupinga kuchaguliwa kwa seneta wa kaunti ya Bungoma Moses Wetangula wamedai kutishiwa maisha yao. Wakili wa Kombo Alfred Ndamabiri amesma mashahidi wa mteja wake wamepokea vitisho kutoka kwa watu wanaodaiwa kufahamika vyema eneo hilo. Hata hivyo, OCPD wa Bungoma Amos Cheboi ameiambia Radio Maisha kwamba hajapokea rasmi malalamishi kutoka kwa wahusika. Kwenye kesi hiyo, Kombo anapinga kuchaguliwa kwa Wetangula kwa misingi kwamba afisa aliyesimamia uchaguzi huo alitangaza matokeo hayo kabla ya kura zote kuhesabiwa.

    0 Responses

    Posted on May 21, 2013 na Mate Tongola

  • Mali ya Umma

    Afisi ya Ruto yatetea ziara yake

    Afisi ya naibu rais William Ruto imetoa stakabadhi za kuthibitisha kuwa ndege aliyokodisha kuzuru mataifa manne ya bara Afrika iliigharimu serikali shilingi milioni 18.5 na wala si shilingi milioni 100 kama ilivyodaiwa. Risiti kutoka kampuni ya VistaJet zinaonyesha kuwa serikali ilikodisha ndege hiyo ya kifahari tarehe 16 na ilisafiri katika miji ya Brazzaville-Libreville-Abuja kabla ya kurejea jijini Nairobi. Aidha, afisi hiyo imetoa stakabadhi zilizowasilishwa na kampuni mbili za ndege; ABM Aviation na LadyLori Kenya ambazo zilidai zaidi ya shilingi milioni 19. Kwa mujibu wa afisi hiyo, iwapo Ruto na ujumbe wake wangesafiri kwa ndege za kawaida, ingewagharimu zaidi ya shilingi milioni 20 na kwamba ziara hiyo ingechukua siku 6 ikilinganishwa na siku 3 walizotumia.

    0 Responses

    Posted on May 21, 2013 na Mate Tongola

  • Usalama

    1 kati ya 6 waliotoroka seli, Tana Delta akamatwa

    Mmoja wa washukiwa sita wa uhalifu waliotoroka kutoka seli ya kituo cha polisi cha Gamba katika kaunti ya Tana River amekamatwa. Bakari Mohammed alikamatwa ijumaa wiki iliyopita nyumbani kwake katika kijiji cha Kiteere, wilaya ya Tana Delta. Mshukiwa alifikishwa mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Garsen Justus Kituku na kukubali mashataka dhidi yake ya kutoroka kutoka kituo cha polisi. Hata hivyo, alikanusha mashtaka ya pili dhidi yake ya kukwepa kukamatwa na polisi. Hata hivyo, Bakari amedai kunyanyaswa na mafisa wa polisi waliomshurutisha kufichua waliko wenzake ambao walitoroka tareh 15 mwezi huu. Mhusika amehukumiwa kifungu cha miaka miwili gerezani.

    0 Responses

    Posted on May 20, 2013 na Mate Tongola

  • Kamati za Bunge

    Jamleck na Ayub Wateuliwa

    Mbunge wa Kigumo Jamleck Kamau ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Kuhusu Kawi. Kamau amemshinda mbunge wa Igembe Kusini Mithika Linturi kwa kupata kura 13 zilizopigwa, huku Linturi akipata kura 10. Aidha aliyekuwa mwanahabari wa Shirika la Standard ambaye sasa ni Mbunge wa Lugari Ayub Savula ameteuliwa bila kupingwa kuiongoza Kamati ya Bunge kuhusu Kilimo.

    0 Responses

    Posted on May 20, 2013 na Geoffrey Mung'ou

  • Usalama

    Visa vya Uhalifu kukomshwa - Uhuru

    Rais Uhuru Kenyatta amewataka makamanda wa polisi kuwachukulia hatua za sheria wale wote watakaohusishwa na vitendo vya utovu wa usalama nchini. Katika mkutano ulioandaliwa katika ikulu ya Rais hapa Nairobi, Uhuru amesisitiza kwamba serikali yake yaitoruhusu utepetevu katika idara ya polisi. Ametoa agizo hilo wkaati kumekuwa na tetesi kwamba baadhi ya wanasiasa wanahusika pakubwa kwenye mashambulizi na mauaji yaliyoshuhudiwa katika kaunti za Busia na Bungoma wiki iliyopita. Duru kutoka mkutano huo wa alhamisi zimearifu kwamba wakuu hao wa polisi walimwarifu rais kuwa wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kazi, kutokuwepo kwa motishia miongoni mwa polisi na kadhalika. Vile vile, mafisa hao wamemtaka rais Uhuru kusitisha mabadiliko yanayofanyiwa idara hiyo ikiwemo kuteuliwa kwa makamanda wa kaunti. Hata hivyo, Uhuru amewahakikishia wakuu hao kwamba atashirikiana nao kikamilifu ikiwemo kushughulikia kwa haraka chamgamoto zinazowakabili.

    0 Responses

    Posted on May 17, 2013 na Mate Tongola

  • Usalama

    Ruto ahimiza vikosi vya AMISOM viongezwe Somalia

    Naibu Rais William Ruto ametoa wito kwa Umoja wa Afrika AU uongeze vikosi vyake vinavyolinda usalama nchini Somalia, AMISOM. Ruto amesema ukosefu wa usalama nchini humo umeathiri pakubwa ustawi wa mataifa mengine ya kanda ya Afrika Mashariki. Ameyasema hayo alipokutana na marais wa Congo Brazzaville Dennis Sassou Nguesso na mwenzake wa Gabon Ali Bongo katika mataifa yao.

    Kwenye mazungumzo yao marais hao wamesema kuongezwa kwa vikosi vya AMISOM nchini Somalia kutaimarisha usalama nchini humo. Haya yanajiri wakati ambapo taifa la Kenya limekabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama yakiwemo mashambulizi ya kigaidi.

    0 Responses

    Posted on May 17, 2013 na Ali Haji Kipapuro

  • Bungeni

    Mzozo wa PAC na PIC wasuluhishwa

    Mzozo uliokumba kubuniwa kwa kamati mbili muhimu za bunge hatimae umesuluhishwa. Wabunge kutoka muungano wa CORD wametangaza kusitisha matakwa yao kuhusu wanachama wa kamati za uekezaji PIC na uhasibu PAC. Sasa Muungano wa CORD umekabidhiwa nafasi 13 katika kamati hizo mbili huku muungano wa Jubilee ukiwa na nafasi 14. Awali, wabunge wa CORD walitangaza kujiondoa kutoka kamati zote za bunge wakishikilia msimamo kuwa lazima Kamati hizo mbili muhimu ziwe na wabunge wengi kutoka upinzani ili kupiga darubini mienendo ya serikali.

    0 Responses

    Posted on May 16, 2013 na Mate Tongola

  • Uslaama

    6 watoroka seli za polisi, Tana River

    Polisi wameimarisha msako dhidi ya washukiwa 6 sugu wa uhalifu waliotoroka kutoka seli ya kituo cha polisi cha Gamba, kaunti ya Tana River usiku wa kuamkia alhamisi. naibu kamishna wa kaunti hiyo Mike Kimoko amethibitisha kisa hicho na kuelezea imani yake kuwa waliotoroka watatiwa nguvuni hivi karibuni. Haya yanajiri wakati kuna tetesi kuwa miongoni mwa waliotoroka ni washukiwa wanne wa mauaji ya watu 38 wakiwemo mafisa 9 wa polisi eneo la Kilelengwani, kaunti hiyo ya Tana River mapema mwezi uliopita. Kis ahiki kinajiri siku mbili tu baada ya wagonjwa 40 wa akili kutoroka kutoka hospitali ya Mathari hapa Nairobi. Hata hivyo, baadhi ya waliotoroka tayari wamerejeshwa hospitalini humo na wanaendelea kupokea matibabu.

    0 Responses

    Posted on May 16, 2013 na Mate Tongola