Mauaji ya simba: Ni nani wa kulaumiwa?

Posted on 22 June 2012 na Kizito Namulanda

Taarifa za wamorani wa jamii ya Maasai kuvamia na kuwaua simba wanne waliokomaa pamoja na wanasimba wawili zimeibua maoni tofauti si humu nchini tu bali hata katika mataifa ya Ulaya. Wengi hasa Wazungu wanaopenda kutalii Kenya kujionea Simba pamoja na wanyama wengine maarufu wanashangaa ni vipi wanyama ambao ni kivutio kikuu watauawa tu hivi kiholela. Baadhi ya Wakenya nao wanawashangaa Wamaasai hao kwa kuwaua wanyama ambao ni kivutio kikuu cha watalii nchini.

 
One of the 6 Lions  killed by Kitengela residents  

Lakini sasa mimi nauliza, makosa ni ya nani? Hebu jiweke mahali pa wamaasai. Umevamiwa na kikosi cha simba hatari ambao tayari wameshawaua mifugo kwa wingi, na sasa wanatishia maisha ya binadamu(hasa wanawake na watoto), utafanya nini? Mmekwisha waarifu maafisa wa Shirika la Wanyama pori lakini hatua haijachukuliwa. Hebu niambie utafanya nini? Utajifungia ndani ya manyatta pamoja na mifungo wako hadi Serikali itakapofika kuwaondoa Simba? Kwa kawaida, lazima utachukua hatua.

Ni msimamo wangu hapa kwamba wa kulaumiwa hapa ni Serikali na bali sio Wamaasai. Serikali ilikuwa wapi kuchukua hatua za haraka kuwaondoa simba mahali wanapoishi watu? Punde baada ya simba hao kuuawa, usiku uliofuatia uliona maangamizi zaidi kwani simba zaidi kutoka mbunga ya wanyama ya Nairobi walivamia boma za wamaasai na kuuwa mifugo zaidi. Sijui Serikali imechukua hatua gani kuzuia uvamizi zaidi?

Hivi sasa Serikali imewatia nguvuni watu kadhaa kutoka jamii ya wamaasai kwa kosa la kuwaua simba. Hii labda ni njia ya kutoa ujumbe kwamba kuwaua  simba na wanyama wengine ambao ni kivutio kwa watalii ni jambo lisiloruhusiwa. Lakini ni nani atakayewatia nguvuni simba kwa kuwaua mifugo wa wamaasai? Ninachosema hapa ni kwamba Serikali inapaswa kuwajibika kikamilifu ili kuzuia utata huu baina ya wanyama wa mwituni na watu wanaoishi karibu na mbuga za wanyama.


 

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining

Nyimbo Zilizochezwa Hivi Karibuni

 
  Mfupi  
  LORD EYEZ PA.mp3  
  Bina na Ngai na Respect  
  Ya Nini Malumbano  
  Nyako Konya  
  News Intro  
  Let's Get down  
  Zanzibar  
  MAISHA ASUBUHI - SOUNDBED  

Video Za Kata Rumba

Skiza Kata Rumba Library2,726 Artists in total
Showing: Overall