Jamleck na Ayub Wateuliwa
May 20, 2013 - Mbunge wa Kigumo Jamleck Kamau ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Kuhusu Kawi. Kamau amemshinda mbunge wa Igembe Kusini Mithika Linturi kwa kupata kura 13 zilizopigwa, huku Linturi akipata kura 10. Aidha aliyekuwa mwanahabari wa Shirika la Standard ambaye sasa ni Mbunge wa Lugari Ayub Savula ameteuliwa bila kupingwa kuiongoza Kamati ya Bunge kuhusu Kilimo. [Soma Zaidi]0 Responses









