Darubini 1.
Serikali Yayumba
Imekuwa vuta nikuvute baina ya walimu na serikali kwa muda wa wiki tatu. Walimu wamegoma kuishinikiza serikali kuwapa nyongeza ya mishahara ili kuwiana na ya watumishi wengine wa umma. Lakini msimamo wa serikali kwamba hakuna fedha za kutosha na hali imetoa nyongeza kwa makatibu huku walimu wakigoma ilifanya hali kuwa mbaya zaidi . Je, kisa ambapo serikali imetoa misimamo mikali ikiwemo kutisha kuwaajiri walimu wapya huku ikibadilisha msimamo na kufanya mkataba na walimu kilikuwa cha kutoa ujumge gani? Ndiyo masuala tunayamulika kwenye Darubini ya upeo huu. Carren Omae anafungua Darubini hiyo.
Posted on September 24, 2012 na Carren Omae
