Wizara ya Usalama
Ole Metito Akabidhiwa Afisi
Waziri mpya wa Usalama wa Humu Nchini Katoo Ole Metito amekabidhiwa rasmi majukumu ya afisi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Yusuf Hajji kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri George Saitoti. Akiwahutubia wanahabari baadha ya kukabidhiwa rasmi afisi hiyo Jumatatu asubuhi, Ole Metito amesema anafahamu changamoto za usalama zinazolikumba taifa hili na kuahidi kuzishughulikia ipasavyo huku akikanusha madai kwamba hana tajriba za kuiongoza wizara hiyo. Metito anachukua afisi hiyo huku kukiwa na changamoto tele zinazoikabili nchi hii ukiwemo ukosefu wa usalama katika baadhi ya maeneo kama vile Tana River ambapo takribani Wakenya 120 wamefariki kutokana na mapigano baina ya makabila mawili. Aidha lipo suala la uvamizi wa mara kwa mara kutoka kwenye kundi gaidi la Al Shaabab. Vile vile anatarajiwa kushughulikia suala la ukosefu wa motisha miongoni mwa maafisa wa polisi hasa kuhusu viwango vya mishahara.
Posted on September 24, 2012 na Geoffrey Mung'ou
