Elimu
Mgomo Wasitishwa Rasmi
Walimu kote nchini wanatarajiwa kurejea shuleni Jumanne saa mbili asubuhi. Muungano unaotetea maslahi yao KNUT hatimaye umetangaza kusitishwa kwa mgomo wa wiki tatu baada ya serikali kusikia malalamishi ya walimu. Katibu Mkuu wa KNUT David Okuta ametangaza hayo Jumatatu adhuhuri akisema walimu ambao ni wanachama wa KNUT wawe shuleni Junanne asubuhi na hivyo shughuli za masomo kuendelea kama kawaida. Katika kikao cha wanahabari baada ya mkutano wa baraza kuu la KNUT, Okuta ameipongeza serikali kwa kutenga kima cha shilingi bilioni 13.5 kufadhili nyongeza ya mishahara ya walimu. Kuambatana na makubaliano yaliyosainiwa Jumapili kati ya KNUT na serikali, mwalimu wa kiwango cha chini atalipwa mshahara wa shilingi alfu 19 tofauti na kiwango cha awali cha shilingi alfu 13. Aidha mwalimu wa kiwango cha juu atalipwa mshahara wa shilingi alfu 134.
Posted on September 24, 2012 na Mate Tongola
