Tana River
Makaburi zaidi yatafutwa Tana Delta
Maafisa wa polisi wanaendelea kuchunguza iwapo kuna makaburi mengine katika msitu wa Ozi, kaunti ya Tana River, siku moja tu baada ya shughuli ya kufukua makaburi mawili yaliyodhaniwa kuwa na miili ya waliouawa eneo hilo kuambulia patupu jana. Mkuu wa polisi mkoani Pwani Aggrey Adoli amedokeza kuwa huenda miili hiyo ilihamishwa kutoka makaburi hayo baada ya waliotekeleza mauaji hayo kuarifiwa kuhusu mpango wa kufukuliwa kwa maiti hizo. Hata hivyo, kuna hofu kuwa huenda miili hiyo ilitupwa katika mto Tana na hivyo kutatiza zaidi uchunguzi wa maafisa hao. Wakati wa shughuli hiyo, ni mguu wa binadamu uliopatikana pamoja na uvundo mkali ishara tosha kuwa kulikuwa na maiti katika kaburi hilo huku polisi wakikadiria kuwa kaburi hilo lilikuwa na miili minne. Haya yanafwatia mzozo kati ya jamii ya wa Pokomo na wa Orma abao umepelekea vifo vya watu 112 katika kipindi cha mwezi moja pekee
Posted on September 21, 2012 na Mate Tongola
