PODCASTS

Habari

  • AJALI YA NDEGE

    31 Akiwamo Waziri Wafariki.

    Waziri wa Dini Nchini Sudan Ghazi al-Sadiq ni miongoni mwa watu 31 waliofariki baada ya ndege iliyokuwa ikiwasafirisha kuelekea jimbo la Kordofan Sudan Kusini kuhudhuria sherehe za Eid ul Fitr kuhusika katika ajali. Kwa mujibu wa msemaji wa mamlaka ya usafiri wa ndege nchini Sudan Abdelhafiz Abdelrahim, ndege hiyo ilikuwa ikielekea katika uwanja wa ndege ulioko Talodi Jumapili saa mbili asubuhi, kabla ya kutokea kwa mlipuko mkubwa ilipokuwa imefika kwenye vilima vya Nuba, hali iliyoiharibu kabisa ndege hiyo. Shirika la habari la Al Jazeera kwa upande wake linasema kuwa mawaziri wawili walikuwa kwenye ndege hiyo. Eneo la Talodi limekuwa ngome ya mapigano yaliyozuka mwezi Juni mwaka 2012 kati ya majeshi ya serikali na wafuasi wa kundi la SPLM.

    0 Responses

    Posted on August 20, 2012 na Geoffrey Mung'ou

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining