Uhifadhi
‘Operation’ Okoa Ndovu
Shirika la uhifadhi wa wanyamapori KWS limetoa wito kwa wakazi wa Narok kuwa makini wakati huu ambapo shirika hilo linapanga kuanzisha shughuli ya kuwahamisha tembo. Ndovu hao takriban 150 wanataarjiwa kuhamishwa hadi katika mbuga ya Maasai Mara kuanzia tarehe 26 mwezi huu. Kulingana na afisa mmoja mkuu wa shirika hilo Partrick Omondi, shirika hilo limeanzisha oparesheni OKOA NDOVU ambayo inalenga kuhakikisha wawindaji haramu wanakabiliwa.
Omondi vile vile ametoa wito kwa wenyeji kuhakikisha wanatoa taarifa kuwahusu watu wanaotekeleza uwindaji wa wanyama hao ambao ni kivutio kikuu cha utalii humu nchini.
Posted on August 18, 2012 na Beatrice Maganga
