PODCASTS

Habari

  • Ushirikiano wa Mataifa

    Kenya yakosoa Sudan Kusini

    Serikali ya Kenya imelalamikia visa vya mauaji ya mara kwa mara yanayotekelezwa dhidi ya raia wa Kenya nchini Sudan Kusini. Wizara ya mashauri ya nchi za Kigeni imevilaumu vikosi vya usalama vya Sudan Kusini kwa kuhusika mauaji hayo ya kiholela. Waziri msaidizi katika wizara hiyo Richard Onyonka amesema kuwa tayari wizara yake imetuma waraka rasmi kwa serikali ya Sudan Kusini ikilalamikia visa ambapo wakenya wanaofanya kazi nchini humo wamekuwa wakiuawa. Takriban wakenya 9 wameuawa katika kipindi cha mwaka mmoja nchini Sudan Kusini. Kifo cha hivi punde ni cha mkenya kwa jina Joseph Matu Mwihia ambaye aliuawa na polisi wa Sudan Kusini kwa madai kuwa hakuwa na leseni ya duka lake la kuuza dawa mjini Juba. Ripoti za serikali zasema kwamba jumla ya wakenya 24 wameuawa nchini humo tangu mwaka 2008

    0 Responses

    Posted on August 17, 2012 na Beatrice Maganga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining