Haki
Mashahidi Wahujumu Kufufuliwa Kesi
Ukosefu wa ushahidi unahujumu juhudi za kufufua kesi zinazohusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu uliopita nchini Kenya.Kwenye mkao wa wanahabri afisini mwake mjini Nairobi naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma Dorcas Oduor amesema kwamba ukosefu wa ushahidi ni moja tu ya changamoto kadhaa zinazozuia kuendelezwa kwa kesi ambazo hazishughulikiwi na mahakama ya mataifa ya jinai ICC. Aidha Oduor amesema bajeti ya idara hiyo haitoshi kufanikisha uchunguzi zaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi. Mapema mwaka huu serikali ilitangaza kufufua kesi 5,000 zinazowahusu watu wanaoshukiwa walishiriki uhalifu wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi mkuu uliopita.
Zaidi ya Wakenya 1,000 waliuawa na wengine zaidi ya laki sita wakifukuzwa makwao kwenye vurugu hizo.
Posted on August 17, 2012 na Mate Tongola
