Darubini 1
Wanapenda Pesa za Wanaume
Yapo madai katika jamii nyingi kwamba jinsia ya kike hupenda zaidi na hata hufurahia fedha ambazo wamepewa kuliko fedha wanazojitafutia wao wenyewe.
Kwamba Mwanamke hata akiwa ameajiriwa kazi daima atafurahia zaidi fedha anazopewa na mumewe kuliko mshahara wake. Inadaiwa kuwa mwanamke hujihisi kupendwa iwapo atapewa fedha na mwanamume. Ndiposa Radio Maisha imetaka kubaini iwapo kasumba hiyo ina mashiko.
Beatrice Maganga ametangamana na wanawake kwa waume ili kubaini uhalisia wa kasumba hiyo.
Posted on August 17, 2012 na Beatrice Maganga
