Somalia
Uchaguzi watarajiwa Somalia-Amisom
Harakati za kupata serikali ya kuongoza taifa la Somalia zimeshika kasi wiki tatu baada ya kupitisha katiba ya muda ya nchi hiyo. Baraza la wazee linalotekeleza majukumu ya bunge linatarajiwa kuongoza shughuli za uchaguzi wa wabunge ambao baadaye watamchagua rais Mpya wa Somalia. Kutokana na harakati hizo Tume ya Umoja wa Afrika Kuhusu Somalia imefanikisha mafunzo kwa wanajeshi 600 raia wa Somalia yaliyoafanyika nchini Uganda. Wanajeshi hao wamewasili nchini Somalia hapo jana na wanatarajiwa kuungana na kikosi cha sasa kuanzisha rasmi idara ya Ulinzi ya serikali mpya ya Somalia. Mwakilishi wa mwenyekiti wa tume ya Afrika kuhusu Somalia balozi Boubacar Diarra ametoa pongezi harakati za uchaguzi wa wabunge na kutoa hakikisho kuwa muungano wa Afrika umejitolea kufadhili harakati za kufaa za amani nchini humo. Amesema muungano wa AMISOM utawapeleka wanajeshi zaidi mjini Mogadishu kulinda amani msimu wa uchaguzi.
Posted on August 17, 2012 na Sofia Chinyezi
