Utetezi
Jaji Barasa akata rufaa
Siku tatu tu baada ya pendekezo la kutimuliwa kwake kutolewa, Naibu Jaji Mkuu Nancy Barasa amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa jopo lililomchunguza. Wawakili wake Kioko Kilukumi amewasilisha rufaa hiyo kwa jopo hilo linaloongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhan ambaye anatarajiwa kuipeleka kwa Mahakama ya Juu Supreme Court. Jumatatu wiki hii, jopo hilo la watu 7 lilimshauri rais Mwai Kibaki amtimue Barasa likisema limempata na hatia ya kutisha kumuua bawabu Rebeca Kerubo na kumfinya pua akiwa eneo lake la kazi. Rufaa hii inatolewa ikiwa imesalia siku 6 tu kwa makataa ya siku 10 aliyopewa kukata rufaa kukamilika.
Posted on August 9, 2012 na Mate Tongola
