Wizi
Mamilioni Yapotea; Mlinzi Azuiliwa
Maafisa wa polisi wanamhoji bawabu mmoja kuhusiana na kupotea kwa mamilioni ya fedha zilizokuwa zikisafishwa kutoka mjini Eldoret hadi jijini Nairobi.
Mlinzi huyo aliyekuwa akisafirisha fedha hizo kutoka uwanja wa ndege wa Eldoret hadi uwanja wa mataifa wa Jomo Kenyatta amedai kuwa fedha hizo ziliibwa baada ya kutekwa nyara na watu asiowajua ambao walimuacha katika mtaa wa Karen. Fedha hizo zinadaiwa kuwa shilingi milioni 45 japo maafisa wa polisi wanasema kuwa shilingi milioni 14 ndizo zilizoibwa. Fedha hizo za Bank of Afrika zilikuwa zikabidhiwe walinzi wa Wells Fargo ambao walikuwa wakizisubiri katika uwanja huo JKIA.
Mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai Francis Muhoro amesema kuwa polisi wanakagua picha zilizonakiliwa na kamera za CCTV ili kuelewa jinsi fedha hizo zilitoweka.
Posted on August 8, 2012 na Beatrice Maganga
