PODCASTS

Habari

  •  

    Darubini 1.

    Masaibu ya Wagonjwa

    Kwa miaka mingi, wagonjwa wengi wakiwamo akina mama wanaojifungua wamekuwa wakifariki mikononi pa madaktari kutokana na utepetevu. Baya zaidi ni suala la wengi wa madaktari kutia kipaumbele ada ya matibabu na hata hongo kabla ya kuwahudumia wagonjwa. Lakini sasa huenda mambo yakabadilika kwa kuwa serikali imeanzisha utaratibu wa kuwashurutisha madaktari kuwahudumia wagonjwa hata iwapo hawana fedha za papo kwa hapo. Tunalichanganua suala hili kwenye darubini yetu adhuhuri ya leo. Geoffrey Mung'ou anafungua darubini hiyo kwa kuangazia masaibu ambayo Wakenya wamekuwa wakipitia wanapotafuta huduma za matibabu, hasa kwa kukosa ada za matibabu.

      0 Responses

    Posted on August 7, 2012 na Geoffrey Mung'ou

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining