PODCASTS

Habari

  • Tanzia

    Mbunge wa zamani ajiua

    Aliyekuwa mbunge wa Turkana kusini Francis Ewaton Achuka amemuua mkewe kwa kumpiga risasi kabla ya kujitoa uhai mapema leo.

    Duru za idara ya polisi zasema kuwa Francis ametekeleza kitendo hicho nyumbani kwake wilayani Lokichar ingawa haijabainika ni nini kilichosababisha mkasa huo. Miili ya wawili hao imepatikana nyumbani kwao na majirani ikiwa na majeraha ya risasi.Polisi wamethibitisha kisa hicho na tayari wamefika eneo la mkasa huku duru zikiarifu kuwa Achuka alikuwa na leseni ya kumiliki bunduki. Wakati huo huo, mkuu wa idara ya upelelezi eneo la Rift Vallet Sameul Nyabengi amesema kuwa wamepokea taarifa hiyo na wameanzisha uchunguzi.Achuka alikuwa mbunge wa eneo hilo kuanzia mwaka 1992 hadi 2007 alipong'atuliwa na mbunge wa sasa Josephat Nanok.

    Mbunge huyo wa zamani atakumbukwa kwa kulitetea eneo bunge lake na hata kuonekana kumzomea aliyekuwa waziri wa barabara wakati huo kwa kutotilia maanani miundo misingi ya eneo zima la Turkana.

    0 Responses

    Posted on August 7, 2012 na Mate Tongola

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining