Uchunguzi
Jaji Barasa kuachishwa kazi
Jopo lililoteuliwa kuchunguza mienendo ya Naibu jaji Mkuu Nancy Barasa limemshauri Rais Mwai Kibaki kumwachisha kazi jaji huyo. Mwenyekiti wa jopo hilo Jaji Mkuu mustaafu wa Tanzania Augustino Stephen Lawrence Ramadhan amesema uchunguzi wa jopo lake umebaini kwamba jaji Barasa alikiuka kanuni za afisi ya jaji kwa kumfinya pua na kumtishia maisha bawabu Rebecca Kerubo. Ikumbukwe kuwa rais Mwai Kibaki alimsimamisha kazi kwa muda Nancy Barasa tarehe 26 mwezi januari mwaka huu na kubuni jopo maalum la kuchunguza mienendo yake. Hatua ya rais Kibaki ilifwatia pendekezo la tume ya huduma za mahakama JSC. Jopo hilo la watu saba linajumuisha, Proffesa Judith Mbula Behemuka, jaju mtaafu Philip J. Ransley, Surinder Kapila, Beauttah Alukhava Siganga, Grace Barbara Ngele Madoka na Profesa Mugambi Jesse Ndwiga Kanyua.
Posted on August 6, 2012 na Mate Tongola
