PODCASTS

Habari

  • Matibabu

    Tiba Kwanza, sio ada-Serikali.

    Serikali imetangaza kwamba Wakenya wote watakuwa wakitibiwa katika hospitali zozote zile hata iwapo hawana fedha za papo hapo za kugharamia matibabu. Kwa mujibu wa kanuni mpya za udaktari wa umma na binafsi, madaktari wote watatia kipaumbele umuhimu wa afya za wagonjwa na wala sio ada za matibabu kama ilivyo sasa. Akitangaza kanuni hiyo mpya, Waziri wa Huduma za matibabu Profesa Peter Anyang’ Nyong’o amesema kanuni hiyo itahakikisha utendakazi bora miongoni mwa madaktari.. Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Githu Muigai ametoa wito kwa madaktari wote kusoma kanuni hizo na kuzielewa.

    0 Responses

    Posted on August 6, 2012 na Seth Onserio

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining