PODCASTS

Habari

  •  

    DARUBINI 1.

    Mkinzano Kuhusu Usajili

    Vinara wakuu serikalini-Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga wanakutana na maafisa wa Tume ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka IEBC ili kutanzua mivutano iliyopo kuhusu mbinu ya kuwasajili wapiga kura. Baadhi ya wanasiasa wanapinga vikali mfumo wa usajili kwa njia ya elektroniki, huku wengine wakiunga mkono wakidai kuwa kutotumiwa kwake kutasababisha wizi wa kura na hivyo kuwa chimbuko la ghasia sawa na zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Ndilo suala tunaloliangazia kwenye sehemu ya pili ya matangazo yetu-Darubini. Geoffrey Mung’ou anafungua darubini yenyewe.

      0 Responses

    Posted on August 6, 2012 na Geoffrey Mung'ou

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining