Olimpiki
Jeptoo aibuka na Fedha Marathon
Mwanariadha Priscah Jeptoo ameishindia Kenya nishani ya Fedha katika mbio za Marathon kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea nchini Uingereza. Jeptoo amenyakua nishani ya Fedha baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa saa mbili dakika 23 nukta 12. Nafasi ya kwanza imemwendea Tiki Gelana wa Ethiopia ambaye ametumia muda wa saa mbili dakika 23 nukta 07 na kuponyoka na nishani ya dhahabu. Petrova Arkhipova wa Urusi ameponyoka na nishani ya shaba baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwa kutumia muda wa saa mbili dakika 23 nukta 29. Licha ya kuanza kwa kasi, Mkenya Mary Keitany amemaliza katika nafasi ya nne kwa kutumia muda wa saa mbili dakika 23 nukta 56. Mkenya mwingine Edna Kiplagat amemaliza katika nafasi ya ishirini. Kwa sasa Kenya imefikisha jumla ya nishani tatu, moja ya Shaba na mbili za Fedha.
Posted on August 5, 2012 na Stephen Mukangai
