PODCASTS

Habari

  • Mashauri

    Clinton aondoka

    Waziri wa Mashauri ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton aliyewasili nchini Kenya jumamosi kwa ziara ya kukutana na viongozi wakuu serikalini ameondoka jumapili asubuhi kuelekea Malawi. Clinton ambaye anaendeleza ziara yake ya siku 11 barani Afrika ambapo atatembelea mataifa saba amefanya mazungumzo na rais Mwai Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga miongoni mwa wakuu wengine na kuwahimiza kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao unakuwa huru na wa haki. Wakati wa ziara hiyo, Marekani iliahidi kuisaidia Kenya katika kupata vifaa vya kuwaandikisha wapiga kura kwa njia ya elktroniki. Ingawa ziara ya Clinton ilisemekana kuwa ya kuimarisha uhusiano wa uchumi baina ya Marekani na mataifa ya Afrika, wachanganuzi wameufasiri kuwa jaribio la Marekani kutaka kupunguza ushawishi wa Uchina unaozidi kukua barani Afrika.

    0 Responses

    Posted on August 5, 2012 na Bernard Oginga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining