Shambulizi
Gruneti yauwa mmoja Nairobi
Mtu mmoja amejilipua mtaani Eastleigh mjini Nairobi alipokuwa akijaribu kuitegua gruneti. Mtu huyo ambaye bado kutambuliwa kwa sababu amepoteza kichwa chake chote alinuia kuwarushia gruneti wanajeshi wanaolinda kambi ya jeshi la wanahewa ya Moi Airbase Eastleigh lakini akashindwa kuitegua. Wanahabari wetu waliofika katika eneo la mkasa wamesema kwamba mtu huyo alikuwa akitoa kipini cha gruneti hiyo kabla kuirusha lakini ikalipuka na kumpasua kichwa. Watu watano wamejeruhiwa ikiwemo mwanajeshi mmoja ambaye amechomeka mkono. Kisa hicho kinaripoti siku chache baada ya mshukiwa mwengine kuwajeruhi watu kadha mtaani humo akitumia mtungi wa gesi.
Posted on August 3, 2012 na Victoria Amunga
