Uchukuzi
Kenya Airways kuwafuta wafanyakazi
Shirika la ndege la Kenya Airways limetangaza mpango wa kuwasimamisha kazi wafanyakazi ili kuajiri wafanyakazi wapya wenye ujuzi uneokwenda na wakati. Shirika hilo linasema uzoefu wa wafanyakazi wa sasa ambao ni zaidi ya 4800 hauambatani na mahitaji ya sasa. Mkurugenzi wa shirika hilo Titus Naikuni amesema mpango huo utatoa nafasi kwa wafanyakazi wanaotaka kustaafu mapema kufanya hivyo. Naikuni amesema bajeti ya kusetiri wafanyakazi katika KQ imeongezeka kutoka shilingi bilioni 6 mwaka 2007 hadi shilingi bilioni 13.4 mwaka huu (2012)
Posted on August 3, 2012 na Tabitha Rotich
