Uchujaji
Jaji Jeane Gacheche atimuliwa
Bodi ya uchujaji Majaji na mahakimu nchini Kenya imemtimua Jaji Jeane Gacheche ikisema hana sifa za kutosha kuhudumu katika idara mpya ya mahakama. Naibu mwenyekiti wa bodi hiyo Roseline Odede amesema kwenye kikao cha kutoa ripoti ya ukaguzi mjini Nairobi kwamba wanachama wa bodi wamepata kwamba jaji Gacheche amekuwa akitoa uamuzi wa mapendeleo kwenye kesi za masuala ya bima. Wakati huo huo Jaji wa Mahakama kuu Lucy Wanjiru Karanja ameepuka shoka la bodi hiyo licha ya kutajwa kuwa Jaji mwenye mihemuko kazini mwake. Bodi imesema licha ya kuwa jaji Wanjiru Karanja anakosa utulivu kazini, sifa zake zingine za kikazi ni nzuri; Bodi imesema sifa zake bora ni kutoa vifungo visivyokandamiza haki za wakosaji. Aidha bodi hiyo imemfaulisha jaji mwengine Jessie Lessit ikisema ikisema amekuwa akiekeleza majukumu yake vyema. Jaji wa mwisho kuepuka shoka la bodi amekuwa ni Mbogholi MSAGHA. Ripoti hiyo ilihusu uchujaji wa majaji wanne ambapo mmoja tu ndiye ametimuliwa
Posted on August 3, 2012 na Alfrique Otieno
