PODCASTS

Habari

  • Atwoli

    Atwoli Kutakiwa Mahakamani

    Huenda Katibu Mkuu wa Muungano wa Wafanyakazi Nchini COTU Francis Atwoli akafungwa gerezani kwa kukiuka agizo la mahakama la kusitisha mgomo wa wafanyakazi wa mashamba ya majani chai. Jaji Isaac Lenaola ameagiza kuwa Atwoli pamoja na maafisa wengine wa COTU wafike mahakamani mwezi Septemba mwaka huu ambapo hukumu dhidi yao itatolewa. Atwoli anadaiwa kuwachochea wafanyakazi wa mashamba ya majani chai ya Kericho kugoma licha ya mahakama kuwaagiza kutofanya mgomo huo. Wafanyakazi hao walikuwa wakilalamikia malipo duni pamoja na mazingira duni ya kufanyia kazi.

    0 Responses

    Posted on August 2, 2012 na Beatrice Maganga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining