Watumishi wa Umma
Wajiuzulu Kufikia Septemba
Watumishi wa umma wenye nia ya kugombea nyadhifa mbalimbali za siasa kwenye uchaguzi mkuu ujao wanafaa wang'atuke ifikapo Septemba 2012. Mahakama kuu imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa mbele yake na mwanaharakati Charles Omanga kupinga makataa ya miezi sita yaliyotolewa na katiba. Katika uamuzi wake Jaji Isaac Lenaola amesema muda huo unatosha kwa watumishi hao kujiondoa na kuanza kampeni zao. Mwanaharakati Charles Omanga aliwasilisha kesi hiyo mahakamani akipinga kifungu cha 43 sehemu ya 5 ya sheria za uchaguzi kuitaka mahakama kuagiza kuwa inakinzana na katiba mpya.
Posted on August 2, 2012 na Sophia Chinyezi
