INFROTRAK
ODM Bado Yaongoza
Matokeo ya utafiti wa hivi punde uliofanywa na shirika la Infotrac Harris yanaonyesha kuwa asilimia 41.9 ya Wakenya wanaunga mkono chama cha ODM na kiongozi wa chama hicho Raila Odinga, asilimia 12. 4 chama cha TNA na kiongozi wa chama hicho Uhuru Kenyatta, asilimia 11.3 wanaunga mkono muungano wa PNU na asilimia 8.1 kuunga mkono chama cha URP na kiongozi wa chama hicho William Ruto. Waliohojiwa pia wana maoni tofauti kuhusu wagombea wenza wa viongozi hawa. Angela Ambitho ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo.
Posted on July 29, 2012 na Zubeida Koome
