PODCASTS

Habari

  • Saudi Arabia

    Wakenya 100 Wakwama

    Zaidi ya Wakenya 100 wamekwama katika kontena moja kwenye ubalozi wa Kenya nchini Saudi Arabia. Katibu katika Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje Thuita Mwangi amesema mpango wa kuwapa hifadhi Wakenya hao umefanywa na serikali. Akizungumza katika kongamano la Wakenya wanaoishi London, mwangi amesema idadi hiyo inajumuisha wanawake 30. Ameitetea serikali kwa kusema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya idadi ya Wakenya wanaokwama nchini humo kuongezeka. Amesema kati ya mwezi Januari na Aprili mwaka huu, zaidi ya Wakenya 200 walilazimika kutafuta usaidizi kutoka ubalozi wa Kenya nchini humo. Amesema hali hiyo imeendelea kuwa mbaya zaidi ikizingatiwa kuwa sheria za nchi hiyo ambazo zinawataka raia wa nje wanaoondoka nchini humo kuwa na visa maalumu kuthibitisha kuondoka kwao. Kwa mujibu wa Mwangi, serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na hali hiyo kukiwamo kupiga marufuku kwa muda usajili wa wafanyakazi kuelekea nchini humo.

    0 Responses

    Posted on July 29, 2012 na Carren Omae

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining