PODCASTS

Habari

  • Ebola

    14 Wafariki.

    Takribani watu 14 wamefariki kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa ebola magharibi ya Uganda. Maafisa wa Shirika la Afya Ulimwenguni wamethibitisha kutokea kwa mkurupuko huo sawa na matokeo ya uchunguzi kutoka maabara ya serikali. Inaarifiwa kuwa visa vya kwanza viliripotiwa katika Wilaya ya Kibaale. Kwa mujibu wa maafisa wa afya nchini humo, 14 kati ya waliofariki ni miongoni mwa ishirini walioripotiwa kupata maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ebola. Hadi sasa hakuna tiba au chanjo ya ugonjwa huo. Mwaka wa 2000 takribani watu 224 walifariki kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo. Mwaka 2007 watu wengine 37 walifariki katika mpaka wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Ugonjwa wa Ebola huenea kwa kasi sana. Miongoni mwa dalili zake ni maumivu kichwani, misuli, kooni, tumboni, kuharisha na kutapika. Kuna wagonjwa ambao pia huvuja damu.

    0 Responses

    Posted on July 29, 2012 na Zubeida Koome

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining