PODCASTS

Habari

  • Mzozo

    Sitamshtaki Miguna, asema Raila

    Waziri mkuu Raila Odinga amesema kuwa hatamshtaki aliyekuwa mshauri wake Miguna Miguna kuhusiana na madai aliyotoa dhidi yake kwenye kitabu chake PEELING BACK THE MASK. Raila amesema hatua aliyochukua ni kuonyesha heshima yake kwa katiba mpya inayompa kila mkenya haki za kimsingi kujieleza bila woga. Kwenye waraka ulioandikwa na mshauri wake wa masuala ya kisheria Paul Mwangi Raila amedokeza kuwa Miguna ana haki ya kikatiba kama mkenya mwengine kujeleza. Bila shaka hatua ya waziri mkuu huenda ikazua mjadala hasa miongoni mwa wale ambao wamekuwa wakisubiri msimamo wake kuhusiana na kitabu PEELING BACK THE MASK. Kwenye kitabu hicho Miguna amedai kuwa Raila ameshindwa kuwachukulia hatua maafisa wafisadi ambao ni washauri wake wa karibu .

    0 Responses

    Posted on July 26, 2012 na Beatrice Maganga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining