Matamshi ya Chuki
Wanasiasa Waonywa
Wanasiasa wameonywa dhidi ya kutoa matamshi yenye chuki na uchochezi katika kampeni zao. Mwenyekiti wa tume ya uwiano na utangamano wa taifa Muzalendo Kibunjia na kamishna wa polisi Mathew Iteere wamesema wanasiasa watakaokiuka onyo hilo watafunguliwa mashtaka. Kwa upande wake kamishna wa polisi Mathew Iteere amewahimiza Wakenya kujifunza kutokana na matukio ya 2007 huku akiwahimia maafisa wa polisi kuwa macho wakati wa kampeni, kura na baada ya kura kuhakikisha vitisho vyovyote vya ghasia vinatibuliwa. Tume ya NCIC imetoa vifaa vya kurekodi kwa siri vitakavyotumika na maafisa wa polisi kunasa sauti za watakaochochea Wakenya ili kusaidia katika uchunguzi.
Posted on July 26, 2012 na Alfrique Otieno
