PODCASTS

Habari

  • Sare

    Mutula aonyesha sketi anayotaka

    Hatimaye waziri wa elimu Mutula Kilonzo amewaonyesha wakenya mfano wa sketi anayopendekeza kuwafaa wanafunzi wasichana katika shule za sekondari. Kwenye kikao cha wanahabari afisini mwake Mutula ametoa sketi hiyo yenye rangi ya zambarau na yenye urefu wa sentimita tatu chini ya magoti. Mutula amewataka wakuu wa shule kushauriana na wizara ya elimu kabla ya kufanyia marekebisho sera mbali mbali za elimu kwenye shule wanazosimamia ikiwemo sare za wanafunzi. Mutula amesema kuwa baadhi ya wakuu hao wamekuwa wakibadilisha sare za shule bila kuzingatia hisia za wanafunzi . Katika siku za hivi karibuni Mutula ameshutumiwa vikali kwa matamshi yake yaliyounga mkono hisia za wanafunzi wa shule moja wilayani Muranga kutaka sare za sketi fupi

    0 Responses

    Posted on July 26, 2012 na Mate Tongola

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining