Ugaidi
Daadaab; Sita wajeruhiwa kwenye Shambulizi
Shambulizi la kilipuzi limetatiza shughuli ya kugawa chakula cha msaada katika kambi ya wakimbizi kaskazini mashariki mwa Kenya. Watu 6 wakiwemo polisi 3 wamejeruhiwa. Kisa hicho kimetukia wakati gari walimokuwa wakisafiria kukigonga kifaa kinachokisiwa kuwa kilipuzi katika kambi ya Dagahaley-Daadab. Watu hao wamejeruhiwa wakiwa kwenye gari la polisi ambalo lilikuwa likiwasindikiza maafisa wa kutoa msaada waliokuwa wakigawa chakula kwenye kambi ya wakimbizi. Aidha maafisa wanane wa kutoa msaada walikuwa wakisafiria gari jingine na hawakujeruhiwa . Mkuu wa polisi mkoani Kaskazini Mashariki Philip Tuimur amethibitisha tukio hilo. Shambulizi hilo limejiri wakati ambapo Kenya imekuwa ikishuhudia misururu ya mashambulizi tangu jeshi la Kenya kuingia nchini Somali kulikabili kundi la kigaidi la Alshabaab.
Posted on July 25, 2012 na Beatrice Maganga
