PODCASTS

Habari

  • NHIF

    Tobiko Abatilisha

    Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Keriako Tobiko amefutilia mbali ombi la Waziri wa Huduma za Matibabu Profesa Anyang’ Nyong'o la kutaka kurejeshwa kazini kwa mkurugenzi wa bodi ya NHIF Richard Kerich. Tobiko amesema kuna uchunguzi unaofanywa na tume ya maadili na kupambana na ufisadi kwa ushirikiano wa maafisa wa polisi kuhusu ubadhirifu wa fedha kwenye hazina ya NHIF na hivyo ni lazima uchunguzi huo ukamilishwe kwanza kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa. Tobiko ameyasema hayo kwenye barua aliyomwandikia Nyong'o. Ni hapo jana tu ndipo Nyong'o alitangaza kumrejesha kazini Kerich.

    0 Responses

    Posted on July 19, 2012 na Beatrice Maganga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining