Ubakaji
Mbelgiji Kizimbani
Mtu mmoja raia wa Ubelijiji aliyenaswa jana akishukiwa kushiriki uroda na wasichana wadogo huku akinasa vitendo vyake kwenye video ameshtakiwa mapema leo katika mahakama moja Mombasa. Allein Robert amefikishwa mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya Shanzu Timothy ole Ntanchu na kushtakiwa kwa kosa la kumbaka msichana wa shule ya msingi. Amekanusha tuhuma hizo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja. Aidha kiongozi wa mashtaka Paul Makonge ameiomba mahakama kuchukua paspoti yake akisema anaweza kutoroka. Hapo Jana Polisi walimtia nguvuni mshukiwa huyo katika eneo la Shanzu baada ya kupatikana na msichana wa darasa la pili katika shule moja ya msingi eneo hilo. Wakazi wa eneo hilo walisema baadhi ya wazazi wamekuwa wakishirikiana na mshukiwa huyo ili wapate fedha.
Posted on July 19, 2012 na Mhariri
