PODCASTS

Habari

  • Siasa

    Napanga Kujiuzulu-Lusaka

    Katibu katika Wizara ya Ustawi wa Mifugo Kenneth Lusaka ametangaza kwamba atajiuzulu wadhifa huo mwezi Septemba ili kujitosa katika ulingo wa siasa. Lusaka ambaye tayari ametangaza azma ya kuwania kiti cha ugavana katika Kaunti ya Bungoma atakuwa katibu wa pili kung'atuka kwenye utumishi wa umma na kujitosa siasani. Wa kwanza kujiuzulu ni aliyekuwa katibu katika Wizara ya Elimu Prof. James Ole Kiyiapi aliyejiuzulu mwezi Aprili na kwa sasa anaendeleza kampeni zake kuwania urais. Lusaka amesema Kaunti ya Bungoma ni mojawapo ya kaunti zenye uwezo mkubwa wa kusitawi kiuchumi iwapo itapata uongozi unaostahiki.

    0 Responses

    Posted on July 19, 2012 na Victoria Amunga

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining