PODCASTS

Habari

  • Miguna

    Sikutoroka Mkono wa Sheria

    Siku moja tu baada ya kuondoka nchini kuelekea Toronto Canada, aliyekuwa Mshauri wa Waziri Mkuu Raila Odinga, Miguna Miguna kupitia mtandao wake wa facebook ameyataja kuwa propaganda madai kwamba ametoroka nchini kukwepa mkono wa sheria, baada ya kukizindua kitabu kwa jina Peeling Back The Mask. Kupitia mtandao huo, Miguna anasema kuwa safari yake haikuwa ya ghafla kwa kuwa alitafuta tiketi ya ndege tarehe 24 Mwezi Mei mwaka huu, huku akielezea kushangazwa kwake na kauli kwamba angesubiri kupewa idhini ya kusafiri na watu fulani. Miguna aliyeondoka nchini Jumatatu mwendo wa saa tano usiku, aidha anadai kuwa alielekea Canada kwa lengo la kukiuza kitabu chache mbali na kujistarehesha na familia yake. Anaongeza kuwa yeye ni mtaalamu wa sheria na kamwe asingekwepa kuyatetea madai yake katika vyombo vya sheria. Anaongeza kuwa hatua ya kutakiwa kutoa ushahidi alio nao ni njia mojawapo ya kuwatishia mashahidi wa kesi za ICC.

    0 Responses

    Posted on July 18, 2012 na Geoffrey Mung'ou

Comments in chronological order (Total 0 comments)



1100 characters remaining