IEBC
IEBC Kuwaajiri Washirikishi
Tume ya Uchaguzi na Mipaka IEBC inapanga mikakati ya kuwaajiri washirikishi watakaohudumu katika maeneo bunge mapya ili kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao unaandaliwa kwa njia ya uwazi. Akihutubu kwenye kikao na wanahabari, kamishna wa tume hiyo Muhammed Allawi amesema tayari nafasi hizo zilitangazwa, na kwa sasa wanakagua barua zilizotumwa ili kuwachagua maafisa hao. Huku hayo yakijiri, idara ya polisi inatarajiwa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi katika kipindi cha miezi michache ijayo kuhusu njia za kuendeleza harakati zao wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Naibu msemaji wa polisi Charles Owino amesema idara ya polisi vile vile itawaajiri maafisa zaidi ili kuhakikisha kuwa usalama unaimarishwa nchini kabla na baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Posted on July 18, 2012 na Beatrice Maganga
